Friday, March 12, 2010

Uchafu Dar

Ukweli ni kwamba jiji letu ni chafu. Nimekua napita maeneo mbalimbali ya jiji letu...inashangaza sana.

Hivi najiuliza...hata usafi majuambani mwetu lazima tufanyiwe na serikali? Ni Kweli kabisa maeneo mengine miundombinu bado sio mizuri. Lakini bado wananchi tunadhamana ya kuhakikisha mzaingira tunayoishi ni masafi.

Si jambo la kustajabisha kukuta magonjwa ya milipuko hasa kipindupindu kinashambulia na kuua. Unaweza kutazama picha hii upande wa kulia hapa. Hili ni eneo la moja Kinondoni,watu wanapika chakula cha mgahawa lakini maeneo yaliozunguka ni machafu kupita kawaida.

Manzese kunatisha,huu ni mfano mmojawapo. Si ajabu watu wa maeno kama haya wakati wote wansumbuliwa na magonjwa ya milipuko.

Pia kuna tabia nyingine isiyopendeza. Badala ya kutumia mapipa ya taka,watu wanazitupa chini!  Na hapa tutataka Manispaa za jiji zitusaidie?

Tutabadilika lini jamani?